Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi, katika khutba za swala ya Ijumaa tarehe 7 Farvardin 1405 (27 March 2026) iliyofanyika katika Muswalla Quds Qom Iram, alisema: Katika siku hizi nyeti na za hatima ambapo tumekabiliwa na makabiliano kutoka katika tabaka mbalimbali na jopo la ubeberu, uelewa sahihi na wa kina wa kauli za kimkakati ni dharura isiyopingika.
Khatibu wa Ijumaa Qom alisema: Katika vita hivi vya mchanganyiko, adui anajaribu kutumia nyenzo za vyombo vya habari na kisaikolojia pamoja na mashinikizo ya nje ili kuleta hali ya kutokuwa na utulivu ndani ya nchi. Katika muktadha huu, wito wa makundi ya wapinzani wa dola ni sehemu ya njama hiyo hiyo ya adui. Lengo la wito huo si kuunda harakati ya kijamii halisi, bali kuvuruga utaratibu wa umma na kueneza taswira ya kutokuwa na usalama.
Alisisitiza: Wananchi kutokuwepo barabarani na askari wa Mungu, kunafungua nafasi kwa askari wa shetani. Ndiyo maana tunasisitiza kuwa; sulama la kutokubakia barabara tupu si ushauri tu, bali ni mkakati wa kumzuia adui.
Mabadiliko ya malengo ya Trump mhalifu kabla na wakati wa Vita vya Ramadhani yanaleta tafakuri.
Kuhusu malengo ya Trump mhalifu kabla na baada ya vita, alisema: Trump na utawala wa Kizayuni wakiwa na malengo kama vile kuangamiza kabisa tasnia ya nyuklia ya Iran, kuangamiza tasnia na nguvu za makombora ya Iran, kuvunja miundo mbinu ya kisiasa, kijeshi na ya ulinzi wa Iran kupitia kumuua kiongozi na mashambulizi mazito dhidi ya miundo mbinu hiyo, kupindua kabisa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuigawa Iran katika sehemu kadhaa zenye bendera tofauti, waliishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Imamu wa Ijumaa Qom alisema: Malengo yao yaliwasilishwa waziwazi kwa sababu hawakuwa na shaka juu ya kufanikiwa kwake. Trump alitaka kutekeleza jambo ambalo lilikuwa ndoto ya miaka 47 ya viongozi wote wa Kizayuni. Walidhani kuwa ndani ya masaa 48 watatimiza malengo yao yote matano na kuimeza Iran pamoja na rasilimali zake zote.
Aliendelea kusema: Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Marekani haikufikia malengo yaliyotajwa, bali imeshurutishwa kufuata malengo mengine, ikiwemo kufungua Mlango wa Hormoz na kurudisha hali ya kawaida ya meli kupita katika njia hii ya kimkakati ya maji, kuzuia kuporomoka kwa masoko ya kifedha na biashara nchini Marekani, kuzuia hasara zaidi za kifedha, vifaa na vifo kwa mali za Marekani huko Asia ya Magharibi, kutafuta njia ya kujitoa katika vita na kuihalalisha mbele ya umma wa Marekani.
Khatibu wa Ijumaa Qom aliongeza kuwa: Uchambuzi linganishi wa makundi haya mawili ya malengo unaonesha kuwa; kiwango cha nguvu za Iran na Marekani katika Vita vya Ramadhani kimebadilika. Dunia, hasa eneo la Asia ya Magharibi, baada ya Vita vya Ramadhani itashuhudia tofauti nyingi za msingi. Kwa mujibu wa mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Magharibi alisema: Iran sasa ni shujaa wa sehemu kubwa ya watu ulimwenguni.
Alikumbushia kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imebaki salama na imepiga hatua chini ya vikwazo vya kidhalimu vya Marekani kwa miaka 47, lakini Marekani baada ya siku chache katika vita na Iran yenye nguvu imejikuta inasalimu amri.
Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ndani ya Qom alisema: Marekani, Magharibi na wote waliokuwa wakitumia Mlango wa Baharari wa Hormoz wafahamu kuwa hali ya Mlango huo kamwe haitarudi katika hali ya kabla ya vita vya kulazimishwa.
Akasema huku akisisitiza kuwa; Iran haitawahi kumpa Trump msaliti ruhusa ya kuamua hatima ya vita: Mataifa mengine yanapokaribia na meli za kivita za Marekani, hupoteza utulivu na kujisalimisha, lakini leo meli za kivita za dola kuu ya dunia zinajificha au kukimbia kutokana na ghadhabu ya makombora yenu enyi watu. Iran inaziita meli za kivita za Marekani mlafi wa dunia zije kwake ili kuzipeleka kwenye kina cha bahari.
Khatibu wa Ijumaa Qom alisema: Vita aliyoianzisha Trump, badala ya kuandaa mazingira ya kubadilisha utawala nchini Iran, imeandaa mazingira ya kubadilisha utawala nchini Marekani.
Maoni yako